AIR TANZANIA NIGHT TEST FLIGHT IN ARUSHA
ARUSHA: Air Tanzania imefanikiwa kufanya majaribio ya safari za ndege wakati wa usiku katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, hatua inayofungua fursa ya kuanza kwa huduma za saa 24.
Majaribio hayo yanaweka msingi wa kuongeza safari za usiku na kutoa fursa zaidi kwa wasafiri wanaofika Arusha nyakati za usiku, huku ikichochea utalii na biashara katika mji huo na maeneo ya jirani pamoja na kuimarisha nafasi ya Arusha kama kitovu muhimu cha utalii na usafiri.
#arusha #FlyAirTanzania #TheWingsofAirTanzania
